Scolastica Msewa – Dar es Salaam.

Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda ameteuliea kuwa Mwenyekiti wa shirikisho la amani duniani – UPF, Kanda ya Tanzania akichukua jukumu la kuhamasisha amani miongoni mwa watanzania bila kubagua dini, dhehebu, mila, Viongozi wa Chama na Serikali, Wabunge na wananchi kuanzia ngazi ya mtu mmoja, familia hadi taifa.

Barua ya utambulisho wa nafasi hiyo, imekabidhiwa kwa mama Pinda na Balozi wa shirikisho la amani duniani bara la Afrika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Amani duniani Kanda ya Afrika –  UPF kutoka nchi ya Ivory Coast, Adama Doumbia.

Kufuatia makabidhiano hayo, Adama ameagiza kuandaliwa kwa sherehe maalumu ya kumtambulisha Mwenyekiti huyo mpya wa ambaye atakabidhiwa rasmi na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mama Marie Kigalu na Viongozi mbalimbali watahudhuria.

Akitoa neno la shukrani, Mama Tunu Pinda ameahidi kuendeleza ushirikiano kwa taifa, bara la Afrika na duniani nzima kutekeleza harakati za kulinda amani kama malengo ya taasisi hiyo yanavyoelekeza.

Amesema, Tanzania ni nchi inayosifika kwa amani na utulivu, hivyo ameahidi kuendeleza kulinda sifa hiyo kwa kutoa elimu katika makundi yote hasa kwa kutumia kundi la tasinia ya Habari na Waandishi wa Habari.

Naye, Kiongozi wa kitaifa wa Shirikisho la Amani duniani Kanda ya Tanzania, Dkt. Stylos Simbamwene amesema suala la amani huanzia na mtu mmoja, familia, Jumuiya mbalimbali, taifa na duniani kwa ujumla.

 

Wengine walipewa Ubalozi wa Shirikisho hilo la Amani duniani katika mikoa mbalimbali nchini kuwa ni pamoja na Dkt. Angella Gloria Bondo, Dkt. Bruno Mwakiborwa, Dkt. Amos Lwitiko Mwakabana, Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga, Archbishop, Aliyekuwa Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Dkt. Alhad Mussa Salum na Julius Lissu Nyenje.

Usafirishaji: Miundombinu haikidhi mahitaji - Mrisho
Dkt. Kimei: Maendeleo? Serikali haina ubaguzi