Uongozi wa Arsenal una mpango wa kumsainisha mkataba mpya Kocha Mkuu wa Mikel Arteta, ili kuongeza chachu ya kumsajili na kisha kumsajili Mshambuliaji kutoka Slovenia na Klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani Benjamin Sesko.

Gazeti la The Mirror limeripoti kuwa, hatua ya Arteta kutarajiwa kusaini mkataba mpya, itatumika kama silaha ya kumvuta Mshambuliaji huyo mwenye umri wa 20, ambaye kwa sasa anaongoza katika orodha ya wanaopigiwa upatu wa kusajiliwa huko Emirates Stadium.

Gazeti hilo limeandika: “Mikel Arteta yuko katika hatua nzuri kukamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya, kufuatia mazungumzo kati yake na Uongozi wa Arsenal kwenda vizuri.

“Mkataba wa sasa wa Kocha huyo kutoka nchini Hispania umebakisha mwaka mmoja, huku akijidhihirisha kuwa mmoja wa makocha wanaochipukia Barani Ulaya.

“Kwa sasa Arsenal wako sokoni kutafuta Mshambuliaji mpya huku Benjamin Sesko wa RB Leipzig akiongoza kwenye orodha iliyowasilishwa mezani kwa viongozi klabuni hapo.”

Bajeti ya Wizara ya ujenzi kutekeleza vipaumbele tisa
Dkt. Msonde: Madai ya Walimu yawasilishwe, yashughulikiwe