Kambi ya matibabu ya moyo kwa watoto wadogo imeanza jkatika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Kambi hiyo ya siku tano inashirikisha madaktari bingwa wa moyo katika Hospitali hii ya Rufaa ya Kanda ya Kati na wenzao kutoka Marekani.

Lengo la kambi hiyo mbali na kutoa huduma ni pamoja kubadilishana uzoefu kwa madaktari katika ubingwa na ubingwa bobezi.

Mamia ya wazazi na walezi kutoka sehemu mbalimbali za nchi wameleta watoto wao kwenye kambi hii ya moyo ya siku tano.

Polisi Moro wafuatilia tukio la raia anayedai kushambuliwa na Askari
Tanga: TRA yaendelea kutoa elimu kwa mlipa Kodi