Lydia Mollel – Morogoro.
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, linafatilia malalamiko yaliyotolewa Wolter Fuime (32), Mkazi wa Mji mwema Mkoani Morogoro anaelalamikia kushambuliwa na Askari Polisi waliokuwa doria Mei 26, 2024 kwenye banda lake la kuoneshea luninga.
Akielezea tukio hilo hii leo Juni 4, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema majira ya usiku Polisi walifika eneo hilo mara baada ya kupokea taarifa fiche kutoka kwa raia wema inayotuhumu kufanyika kwa matendo yaliyo kinyume na maadili ikiwemo kuonyesha picha zisizo na maadili kwa watoto wadogo.
Amesema, lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituoni na baadae kuachiliwa kwa dhamana kwani baada ya mtuhumiwa kuachiliwa kwa dhamana alililalamika kuwa anaumwa hiyvo anaomba hati ya kutibiwa.
Mkama ameongeza kuwa kila hati ya matibabu inayotolewa na Jeshi la Polisi lazima uchunguzi ufanyike hivyo jeshi hilo mkoani Morogoro linaendelea na uchunguzi wa swala hilo hili kubaini ukweli na endapo uchunguzi utakamilika taarufa kamaili itatolewa
Sanjari na hayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa makosa ya mauaji katika wilaya ya kilombero na kilosa.
Hata hivyo, Kamanda Mkama ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari zidi ya wenza wao kwani matukio yote tajwa yamesababishwa na sababu kadha wa kadha ikiwemo imani za kishirikina, tamaa ya mali na migogoro ya kifamilia.