Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji- EWURA, inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini ambazo zimeanza kutumika kuanzia hii leo  Jumatano Juni 5, 2024 huku kwa Mkoa wa Dar es Salaa Petroli ikiwa ni Shilingi 3,261 Dizeli Shilingi 3,112 na Mafuta ta taa Shilingi 3,261 bei ambazo zimepungua kwa wastani wa asilimia 11.82
kwa mafuta ya Petroli, asilimia 7.77 kwa mafuta ya Dizeli na asilimia 7.94 kwa Mafuta
ya Taa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurukenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule imeeleza kuwa mabadiliko hayo ya bei za mafuta kwa mwezi Juni 2024 yamechangiwa na kupungua kwa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB), huku Wafanyabiashara wakitakiwa kuzingatia uuzaji wa Nishati hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166.

Aidha, EWURA imesema Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa bonyeza hiyo link hapo chini.

Cap-Prices-for-Petroleum-Products-wef-5th-June-2024-Kiswahili

 

 

Dkt. Jafo ahimiza upandaji wa Miti kwenye vyanzo vya Maji
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Juni 5, 2024