Wito umetolewa kwa watu wenye ualbino kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kupata huduma za afya iliwaweze kunufaika na fursa mbali mbali zinazotolewa na serikali ikiwemo vipimo na mafuta kinga bure kwaajili yao.

Hayo yamesemwa na Daktari wa Kinga ya Magonjwa ya saratani wa taasisi ya Ocean Road, Dkt Maguha Stefano wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha Mkoani Pwani kwenye kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya kuongeza uelewa juu ya ualbino duniani katika viwanja vya Mailmoja kibaha mkoani Pwani.

Alisema wanaofika hoispitalini hapo ni wachache hivyo amewataka watu wenye ualbino kujitokeza kwa wingi hospitalini hapo ili waweze kuhudumiwa huduma mbali mbali kwa usalama wa maisha yao na kwamba taasisi hiyo imekuwa ikitoa elimu katika maonyesho ya maadhimisho hayo ambapo wamewapa elimu ya kujiepusha na kukaa muda mrefu kwenye jua ili wasipatwe na saratani ya ngozi ambayo imekuwa ikiwashambulia zaidi.

“Lakini pia tumeweza tunawashauri kuwa na tabia ya kupima afya yao ya ngozi mara kwa mara kwa kufika taasisi ya saratani ocean Road ambao huwa tuna kliniki ya ngozi kwa watu wenye ualbino kila alhamisi hivyo wawe wanakuja kila ambavyo wanashauriwa na Daktari ambapo angalau waje kila baada ya miezi sita kucheki afya za ngozi zao,” alisema Daktari Maguha.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Kinga wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Daktari Chrispin Kahesa amesema taasisi hiyo imejiwekea mkakati maalumu wa kufikia jamii kwa kutoa elimu mashuleni, tiba za awali kwa kushirikiana na taasisi ya watu wenye ualbino nchini TAS ambao wameandaa mtaala maalumu ya utoaji wa elimu.

Alisema wanazunguka katika shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini kutoa elimu walitoa elimu ya taadhari ya kupata saratani ya ngozi na kuwapa nasaha ya kuona jinsi gani watapunguza kuweza kuongezeka kwa saratani ya ngozi.

Ujenzi Barabara ya lami Katavi - Kigoma wafikia asilimia 60
MALIMWENGU: Ajizushia kifo ashuhudie watakaofika msibani