Ama kweli Ulimwengu umejaa vituko. Kuna tukio la mwaka 2007, ambapo Raia wa Bosnia, Amir Vehabovic (45), alidanganya kuwa amekufa, ili kuona ni watu wangapi wanamthamini na ambao watahudhuria mazishi yake.

Amir alitengeneza mtu bandia anayefanana naye ambaye alimlaza kwenye jeneza, kisha yeye kuvaa sura bandia iliyombadilisha muonekano ili asiweze kujulikana akijifanya rafiki wa marehemu.

Siku ya mazishi iliwadia huko kusini mwa Bosnia katika mji wa Gradiska, lakini cha ajabu msibani walikuwepo watu wawili tu, yaani mama yake na yeye mwenyewe kwani hakuna rafiki wala ndugu wengine waliofika.

Amir alisikitika sana, kisha akaandika barua ya kuwakashifu ndugu, jamaa na marafiki wote wapatao 45 ambao hawakujitokeza licha ya kupata taarifa za msiba huo na kuelezea uhalisia wa tukio lile.

Aliandika kuwa, “Hivi mnajua nililipa pesa nyingi kupata cheti feki cha kifo na nilitoa rushwa ili kupata jeneza tupu.”

“Niliwaza sana kuhusu ninyi mnaojiita marafiki zangu, mngejitokeza tu kutoa heshima zenu za mwisho. Sasa nimejionea ni nani naweza kumtegemea,” alimaliza Amir.

Ama kweli Dunia haiwezi kwisha vituko, halafu kumbe mambo haya yalianza kitambo sana na ni wazi kiwa hakuna jipya chiji ya jua, ila sipati picha ingekuwa kibongo bongo hali ingekuwaje.

 

Wenye ulemavu wa ngozi waitwa Ocean Road
Wiki ya Utumishi: TASAF kuwajengea uelewa Wananchi