Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mfumo katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Japhet Boazi amesema katika wiki hii ya utumishi wamejipanga kuhakikisha wanajenga uelewa kwa Wananchi tofauti tofauti.

Akizungumza hayo hii leo Juni 19, 20224 katika maonesho ya Wiki ya utumishi Nchini yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma, amesema mpango wa TASAF umeleta mabadiliko mengi sana katika jamii, na inawanufaikaji wengi walio nufaika na mfuko huo.

“Wiki hii ni fursa nzuri ya kufikisha ujumbe na wale wote wenye malalamiko tutawasikiliza na kuzipatia ufumbuzi. Hapa tupo kwaajili ya Wananchi wote wenye kutaka kujua mfuko huu lakini pia wwnye changamoto mbali mbali tutazitatua kqa kadri tuwezavyo,” alisema Boazi

Naye Mnufaika wa mfuko huo, Umukuruthumu Abdalah amesema TASAF imemfungulia njia katika kufikia malengo yake ambayo alitamani kufikia.

MALIMWENGU: Ajizushia kifo ashuhudie watakaofika msibani
Idris Sultan uso kwa uso na Osimhen