Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla ameongoza Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki Bonanza la CRDB BUNGE Grand Bonanza lililofanyika katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma hii leo 22 Juni, 2024.

Bonanza hilo limehudhuliwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

Michezo mbalimbali iliyofanyika katika bonanza hilo ni Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, kupokezana vijiti, kufukuza Kuku, kula, kunywa soda, kukimbia na gunia, mbio za riadha nk.

Dhumuni kuu la bonanza hilo ni kuwezesha ujenzi wa shule ya sekondari ya Bunge wavulana (Bunge Boys), kujenga afya pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali.

Utambuzi wa haki: Vikundi vya Hisa Kuwasaidia Watu wenye ulemavu
Ujenzi Barabara ya lami Katavi - Kigoma wafikia asilimia 60