Uwepo wa huduma mbovu katika Baadhi ya ofisi za Serikali pamoja na Taasisi mbalimbali nchini Tanzania umetajwa kusababishwa na kukosekana kwa muda maalumu wa Kuwapa nafasi za kupumzika watumishi wa kada za Watunza kumbukumbu, waandishi waendesha ofisi (PS) pamoja na wahudumu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mvomero, Said Nguya alipokuwa akizungumza na watumishi wa kada hizi katika ziara maalumu ambayo iliyoandaliwa Wilaya ya Mvomero ikiwa pia ni katika juhudi za kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutangaza utalii wa ndani.

Amesema kuwa watumishi hawa ndio moyo wa Ofisi lakini wameonekana kusahaulika katika utumishi wao na kukosa muda wa kutosha wa kupumzika na kuwaongezea hamasa kwa kupata fursa ya kuchangamana na kubadilishana uzoefu miongoni mwao kama zifanyavyo Kada zingine.

Katibu Tawala Wilaya ya Mvomero, Said Nguya.

Kwa upande wake Kaimu Mhifadhi, David Kadomo ameridhishwa na kitendo kilichofanywa na Wilaya ya Mvomero hivyo ameziomba Halmashauri na Wilaya zinigne kuiga mfano huu kwani kunawapa faida watumishi hawa na kuonekana wanakumbukwa muda wote.

Nao baadhi ya watumishi waliohudhuria katika ziara hii wamempongea katibu tawala kwa uamuzi mzuri alioufanya juu Yao na imewapa nguvu ya kufanya kazi kwani Jambo hili halijawahi kufanyika sehemu yoyote ile

Ziara hiyo maalum, imefanywa na Katibu Tawala Wilaya ya Mvomero akiongozana na watumishi wa kada za Watunza kumbukumbu waandishi waendesha ofisi (PS) pamoja na wahudumu katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni katika jitihada za kutangaza utalii wa ndani.

Dkt. Jafo: Serikali imeweka mazingira wezeshi kibiashara
Mfuko wa pamoja: Sillo awapa tano Wanahabari Manyara