Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi, Vladimir Putin juu ya amani ya mataifa ikiwemo suala la Urusi na Ukraine.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Jijini St. Petersburg nchini Urusi hii leo Julai 12, 2024 Dkt Tulia na Putin wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha amani Duniani.
Kuhusu mgogoro unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Dkt. Tulia amesema “Kabla ya kuzungumza naye tayari tulishazungumza na Maspika wa nchi zote hizo mbili na sisi kama Umoja wa Mabunge Duniani.”
“Tumezungumza naye kama Kiongozi wa nchi katika sura ambayo tunaweza kuziweka pamoja nchi zote mbili na tutarajie kwamba IPU itatengeneza fursa ya Mabunge ya pande zote ili kuweza kuzungumzia amani katika maeneo yao ya utawala,” alisema Dkt.Tulia.
Akizungumza katika majadioiano hayo, naye Rais Putin amesema, “Bi Ackson, kwanza nikushukuru kwa Mjadala wa Wabunge wa Wabunge wa BRICS. wajumbe 400 kutoka nchi 18 wanashiriki hatua hiyo na hii bila shaka inaonyesha kwamba BRICS na ushirikiano wa bunge wa BRICS wanafurahia maslahi makubwa na kuongezeka kwa imani kutoka jumuiya ya kimataifa. Hili linaeleweka, kwa sababu kanuni za BRICS hufanya kazi –usawa wa kweli.”