Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Kibiti imezitaka taasisi za serikali kufanya kazi pamoja ilikusaidia miradi kukamilika kwa wakati hasa ikizingatiwa taasisi zote za serikali utendaji wake unategemeana.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaruke wakati akiwa katika Kijiji cha Nyanjati wakikagia utekelezaji wa ilani wa miradi ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Wilaya ya Kibiti katika miradi ya REA na TANESCO
Amesema utekelezaji kazi wa shirika la Umeme TANESCO unategemeana na TARURA kwa Barabara zake inazojenga na pia TANESCO na TARURA wanategemea huduma ya RUWASA katika kuwahudumia Wananchi.
“Kwa mfano TANESCO, RUWASA na TARURA iwapo mkizungumza lugha Moja katika utendaji wa pamoja katika kutekeleza miradi tutatatua kero za Wananchi kwa haraka zaidi” alisema Ndaruke.
ziara hiyo Ina lengo la kutaka kujionea hatua za utekelezaji wa miradi hiyo na namna wanavyoendelea na utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha ameagiza Wakandarasi kutoa kipaumbele Cha kazi zao kuanza kutekeleza miradi ya mkoa wa Pwani kwanza ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati iwapo watakuwa na kazi za miradi katika mikoa mingine.
Na pia aliwataka Wakandarasi hao kutumia nguvu kazi za vijana waliopo vijijini kwenye miradi ya umeme ili watoe ajira kwa vijana sawa na agizo la ilani ya CCM.
Meneja wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO Eng. Safari Kwibondoja amesema miradi hiyo ni mkakati wa kufikisha Umeme katika shule za Sekondari Samia, mradi wa kufikisha Umeme zahanati ya Majwa na mradi wa kufikisha Umeme katika pamp ya maji ya Kijiji cha Nyanjati.
Amesema miradi hiyo itasaidia kusogeza huduma za uhakika sekta ya afya, kumtua mama ndoo ya maji kichwani ambapo maji yatapatikana kwa gharama ndogo tofauti na ilivyo Sasa na kuboresha utoaji wa elimu katika shule ya Sekondari Samia.
“Lakini kingine kusaidia Wananchi kufanya shughuli za Maendeleo hasa kujiongezea kipato kwa kujiajiri kupitia huduma ya umeme utakaopatikana baada ya miradi hiyo kukamilika.
Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibiti imekagua miradi ya umeme REA na TANESCO yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 202 ikiwa ni kuchagua utekelezaji wa ilani ya CCM kuhakiki Maendeleo ya miradi ya kufikisha Umeme kwenye huduma za jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph kolombo amesema miradi hiyo ni mikubwa na muhimu kwa Wananchi amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha hizo na kuagiza miradi hiyo ikamilike haraka kabla ya mwezi Desemba mwaka huu iwe imekamilika.
Aidha Kanali kolombo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kuharakisha uwekaji Umeme katika shule ya Sekondari Samia ambayo tayari TANESCO wameshafikisha Umeme hadi eneo la shule hiyo.