Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Prof. Kabudi anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Pindi Chana ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.