Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akichukua nafasi ya Jaji Dkt. Eliezer Feleshi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo, Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), ambapo pia Rais Samia amemteua Samwel Maneno kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Maneno alikuwa Msaidizi wa Rais, Sheria na sasa anachukua nafasi ya Balozi Prof. Kennedy Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Sheria na Mikataba.
Aidha, Rais Samia pia amemteua Dkt. Ally Possi kuwa Wakili Mkuu wa Serikali, ambapo kabla ya uteuzi huo, alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.