“Tumeweka historia – wafuasi BILIONI 1! Hii ni zaidi ya nambari tu – ni ushahidi wa shauku yetu ya pamoja, ari na upendo kwa mchezo na kwingineko. Kuanzia mitaa ya Madeira hadi hatua kubwa zaidi ulimwenguni, nimekuwa nikiichezea familia yangu na wewe kila wakati, na sasa bilioni 1 kati yetu tunasimama pamoja. Umekuwa nami kila hatua ya njia, katika hali zote za juu na za chini. Safari hii ni safari yetu, na kwa pamoja, tumeonyesha kuwa hakuna kikomo kwa kile tunaweza kufikia. Asante kwa kuniamini, kwa msaada wako, na kwa kuwa sehemu ya maisha yangu. Bora zaidi bado zinakuja, na tutaendelea kusukuma, kushinda, na kutengeneza historia pamoja.”

Hayo ni maneno ya Cristiano Ronaldo aliyoyaandika kwenye mitandao Yake ya Kijamii mara baada ya kufikisha wafuasi bilioni 1 kwenye mitandao Yake ya Kijamii na kufanya nyota huyo kuandika historia mpya duniani.

Ronaldo ameweka rekodi ndani na nje ya uwanja. Nyota huyo ndiye mchezaji pekee duniani aliyefikisha rekodi ya kufunga mabao 900 akiwa na timu mbalimbali. Mfungaji Bora wa taifa la ureno na michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa nyakati zote.

Nje ya uwanja Ronaldo anawafuasi wengi mno kuanzia mtandao wa Instagram,x, Facebook,tiktok na YouTube. Mafanikio haya makubwa yamejengwa kwa miaka 19 Akiwa kama mchezaji

Singida BS yaishusha Simba kileleni
Watakiwa kujenga mahusiano mazuri na Wananchi