Wafanyakazi wa Urusi walipewa likizo ya kufanya ngono leo ili kuongeza kiwango cha kuzaliwa, siku hii ilitangazwa kuwa Siku ya Mimba huko Ulyanovsk, ambapo wanandoa waliambiwa waende nyumbani ili kupata muda wa kuongeza uzao.
Ili kufanikisha jambo hili, walitangaziwa zawadi ya kushinda gari, pesa taslimu au friji, chini ya mpango wa baraza la jiji la “Zaa kwa Patriot”, kwa wale ambao wangejifungua Juni 12, ambayo ndiyo siku maalum kwa Urusi kwa tukio hilo na wengineo pia wangepata tuzo.
Wanandoa walioshinda zawadi kuu (gari la 4×4), lililotengenezwa ndani ya nchi hiyo, watapitishwa kwa vigezo vya Kamati ya kama vile “heshima” na “malezi ya kupongeza” mpango ambao ulisimamiwa na Gavana wa Ulyanovsk, Sergei Morozov.
Septemba 12, 2006 ndipo Rais wa Urusi alihutubia taifa hilo na kutangaza janga la idadi ndogo ya watu kuwa ni tatizo la dharura na akatangaza jitihada za kuongeza kiwango cha idadi ya watu na kuongeza uzazi nchini Urusi.
Alisema Serikali ingetoa motisha ya pesa taslimu kwa familia ambazo zina zaidi ya mtoto mmoja, ili zihamasike kuongeza watoto, ndipo siku hiyo ya Septemba 12 kila mwaka ikawa ni siku muhimu ambayo ilipewa heshima kama ‘siku ya kupeana ujauzito kwa raia wa Urusi.
Badaye Serikali ikaanzisha siku ya mapumziko kwa umma, ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kuwapa wanandoa muda wa faragha kwa matumaini kwamba watashika mimba na Wazazi ambao watoto wao huzaliwa miezi tisa baadaye wakapewa fursa ya kushinda zawadi hizo na Watoto wanaozaliwa Septemba 12 hupata zawadi kutoka kwa Mamlaka.
Tangu mpango huo uanze, kiwango cha kuzaliwa katika eneo hilo kiliongezeka, ikikumbukwa kwamba kupungua kwa viwango vya kuzaliana, kuongezeka kwa wahamiaji na watu kwenda nchi zingine, mfumo dhaifu wa huduma ya afya na mambo mengine yalichangia tangu kuanguka kwa Soviet mnamo 1991.