Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhani amewaasa wananchi kujitokeze kupiga kura kuwachagua Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa, Kijiji au Kitongoji, Wajumbe wanawake na wajumbe mchanganyiko katika maeneo yao kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika nchini.
Kailima amtoa nasaha hizo baada ya kupiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Chadulu kilichopo Kata ya Makole katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma hii leo Novemba 27, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo nchini.
Amesema, zoezi la kupiga kura halichukui muda mrefu kwani ndani ya dakika mbili unakamilisha haki ya kikatiba kuchagua viongozi katika uchaguzi huo.
Aidha, amewasihi Watanzania na wapiga kura wa mtaa wa Chimuli II kufika kwenye vituo vya kupigia kura na kutekeleza haki yao ya kikatiba.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika leo nchini baada ya wiki moja ya kampeni za uchaguzi na vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa 2.00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni.