Chelsea na Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle Alexander Isak, Manchester United yaarifiwa kuhusu hali ya kandarasi ya Alphonso Davies Bayern Munich na Graham Potter auliziwa na Wolves na West Ham.
Arsenal na Chelsea zinamtafuta mshambuliaji na klabu hizo mbili za London zina orodha sawa ya wachezaji wanaowataka, ambayo ni pamoja na mshambuliaji wa Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 25. (Caught Offside)
Manchester United pia imefanya usajili wa mshambuliaji kuwa kipaumbele chake katika uhamisho la Januari. (Mirror)
Bayern Munich wanajiandaa kumuongeza mkataba wa mchezaji wao wa kimataifa wa Canada Alphonso Davies, huku Manchester United wakifahamu kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 24 huenda akasaini mkataba mpya licha ya kumtaka. (Floran Plettenberg, Sky Germany)
Manchester United wako nyuma ya Chelsea katika kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa Lecce raia wa Denmark Patrick Dorgu. (Team Talk)
Kocha wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter ameuliziwa na klabu za Wolves na West Ham. (Sportsport)
Kocha wa zamani wa Borussia Dourtmund Edin Terzic hatakuwa mkufunzi mpya wa West Ham ikiwa Lopetegui ataondolewa kwenye nafasi yake, lakini mkufunzi wa zamani wa Denmark Kasper Hjulmand yuko kwenye kinyang’anyiro. (Florian Plettenberg)
Kocha wa zamani wa West Ham David Moyes ni miongoni mwa wanaowania nafasi ya kazi katika klabu ya Wolves iwapo Gary O’Neil atafukuzwa (Telegraph – usajili unahitajika)
Liverpool wanawasiliana na Bayer Leverkusen kuhusu uhamisho wa beki wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 23. (Caught Offside)
Manchester City itamruhusu kiungo wa Ubelgiji Kevin De Bruyne, 33, kujiunga na moja ya vilabu dada vya City Football Group atakapoondoka kwenye kikosi cha Ligi ya Primia. (Telegraph – usajili unahitajika)
Lakini Inter Miami ya David Beckham imemfanya De Bruyne kuwa shabaha yao kuu ya uhamisho. (Mirror)
Mshambuliaji wa Everton na Guinea-Bissau Beto, 26, na kiungo wa Mali Abdoulaye Doucoure, 31, wanasakwa na klabu ya Roma. (Gazzetta dello Sport kupitia Football Italia)
Liverpool wana uhakika mlinzi wa Ufaransa Ibrahima Konate, 25, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo huku mazungumzo yakiendelea kuhusu mkataba mpya. (Fabrizio Romano)
Juventus na Marseille wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Mfaransa Benoit Badiashile. (Caught Offside)
Chelsea imefanya mawasiliano na klabu ya Benfica kuhusu mpango wa kumsajili beki wa Ureno Tomas Araujo, 22, huku klabu hiyo ya London ikiwa tayari kumruhusu mlinzi wa Ufaransa Axel Disasi, 26, kuondoka mwezi Januari. (Team Talk )
Mustakabali wa Fabio Vieira wa Arsenal katika klabu hiyo uko mashakani huku The Gunners wakiwa tayari kupokea ofa ya kumuuza kiungo huyo wa kati Mreno mwenye umri wa miaka 24, ambaye kwa sasa yuko Porto kwa mkopo. (Daily Mail – usajili unahitajika)
Mkurugenzi wa kandanda wa Barcelona Deco amekutana na wawakilishi wa beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 28, ambaye mkataba wake katika klabu ya Bayer Leverkusen unamalizika msimu ujao. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)