Klabu ya Yanga inarejea dimbani leo hii kuwavaa JKT Tanzania mchezo wa Ligi kuu NBC utakaopigwa dimba la Meja Generali Isamuyo saa 10:15 jioni. Huu utakuwa mchezo wa raundi ya 18 kwa JKT Tanzania na Yanga. Mchezo huo unategemewa kuwa na ushindani kutokana na rekodi mbalimbali
JKT Tanzania
Wanashika nafasi ya 10 wakiwa na alama 19katika michezo 17 waliyocheza.Kama wataiobuka na ushindi watafikisha alama 22 na kupanda mpaka nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi. Mchezo wa raundi ya 17 walivaana na Coastal Union na wakaishia kupoteza kwa mabao 2-1.
Katika mkutano na waandishi wa Habari kocha Ahmad Ally alinukuliwa akisema”Tunahitaji kuwa Bora zaidi uwanjani kwani tunacheza na timu bora hivyo tutahakikisha tunakuwa watulivu na Bora kuliko wapinzani tukiwa na mpira na hata bila ya mpira”
YANGA
Kwa sasa Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na alama wakiwa na alama 45 baada ya michezo 17. Yanga wanapaswa kushinda mchezo huo ili kuendelea kuongoza ligi na kupunguza ushindani kwa wapinzani wao Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 44. Mchezo uliopita dhidi ya Ken Gold waliibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 na kuongeza ari ya ushindani kwa timu hiyo. Naye Kocha mkuu Miloud Hamdi amenukuliwa akisema
”Ni kweli mchezo uliyopita tumefunga magoli 6 na ni kwa sababu tunakikosi bora ,Jukumu letu ni kuhakikisha tunafanya vizuri kila mchezo ,nina imani kubwa kwa wachezaji wangu na tumezungumza kuwa kwa sasa kitu muhimu ni kupata pointi 3 na sio idadi ya magoli”
”Tunatambua kuwa kesho tutakuwa na mchezo mgumu lakini tutafanya juhudi kubwa kuhakikisha tunapata alama tatu,nawafahamu JKT Tanzania ni timu nzuri na wanapenda kucheza vizuri hivyo sisi tunajiandaa kucheza vizuri ili kupata alama tatu”