Watafiti wa Afya wa Taasisi ya Robert Koch – RKI, ya Ujerumani, wamesema kwa mwaka huu pekee (2023), takriban watu 3,100 wamekufa kwa joto kali.
RKI inasema, idadi kubwa ya waliopoteza maisha ni watu wenye umri miaka 75 au zaidi, huku utafiti huo ukionesha kuwa Wanawake hufa zaidi kuliko wanaume kutokana na joto, kwa kuwa kuna na idadi kubwa ya wanawake miongoni mwa wazee.
Aidha, rekodi za taasisi ya RKI pia zinaonesha vifo vinavyohusiana na joto nchini Ujerumani kufikia watu 6,000 katika miaka ya 2018, 2019 na 2015.
Hata hivyo, RKI inasema katika miaka ya 2014, 2016, 2017 na 2021, kulikuwa na vifo kati ya 1,000 na 1,700.