Mamlaka ya nchini Ureno, imebainisha wimbi la joto kali linaloendelea kushuhudiwa katika mataifa ya Mediterania limesababisha vifo vya watu 238 kufikia sasa.

Maelfu ya wataalamu wa zimamoto, wanaendelea kukabiliana na janga la moto katika nchi za Ureno, Hispania na Ufaransa ambalo linasababishwa na joto kali.

Moto umekuwa ukiteketeza maeneo ya kusini-magharibi mwa Mkoa wa Gironde nchini Ufaransa, ambapo zaidi ya watu 12,000 wamehamishwa.

Wazima moto na watu wa kujitolea wakijaribu kuzima moto wakati wa joto nyikani kwenye kijiji cha Kineta, karibu na Athens Ugiriki.

Kaskazini mwa Ureno, rubani mmoja aliangamia wakati ndege yake ya kusaidia shughuli za zima moto ilipoanguka katika eneo la Foz Coa, karibu na mpaka wa Hispania.

Ongezeko la joto kali, limekuwa likishuhudiwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na shughuli za binadamu.

Kwasasa, joto Duniani limeongezeka kwa takriban nyuzi joto 1.1C tangu enzi ya viwanda ianze na halijoto itaendelea kuongezeka iwapo mataifa kote ulimwenguni hayatafanya juhudi za kupunguza kiwango cha uzalishaji wa kaboni.

Majira ya joto yaliyosababisha Wananchi kukimbilia ufukweni.

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Ufaransa, Gerald Darmanin alisema kufikia sasa moto umeteketeza hekta 10,000 (ekari 25,000) za ardhi.

Joto hilo, limekuwa likipanda tangu Jumanne hadi kufikia nyuzi joto 47 nchini Ureno na zaidi ya nyuzi joto 40 nchini Hispania, na kusababisha ukame na ukavu unaochochea moto.

Watabiri wa hali ya hewa wa Ureno, wanasema joto kali litaendelea kupanda juu ya nyuzi joto 40 kabla ya kushuka wiki ijayo.

Waangalizi uchaguzi 'wamulika' kampeni Kenya
Rais amfuta kazi Mkuu wa Ujasusi