Baada ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza wagombea wake kwa nafasi za ubunge,udiwani na uwaakilishi kuanza kuchukua fomu tarehe 14 julai mwaka huu, hali katika ofisi za chama hicho manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera zimeonekana kujaa watiania wanaochukua fomu kwaajili ya kuwania nafasi za ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini ambao wamefikia 36.
Miongoni mwa waliofika katika ofisi hizo na kuchukua fom ni wakili Allon Kabunga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea kanda ya Kagera ambaye amesema kuwa licha ya kuwa yeye ni wakili laki pia ni mwanachama hai wa chama hicho hivyo baada ya kujipima ameona anatosha kuwatumikia wanabukoba mjini kupitia ubunge.
Ameeleza kuwa msimu huu chama kimewapa nafasi kila mwananchama anayejua anatimiza vigezo kugombea nafasi yoyote ikiwa ni demoklasia hivyo ameona anayohaki ya kuchukua form na kugombea na matumaini yake ni kwamba chama kikimpitisha basi ataweza kuipeperusha vyema bendera katika uchaguzi mkuu.
Wengine waliochukua fomu ni mfanyabiashara maarufu Audax Kaijage maarufu Omujumba ambaye pia aliwahi kuwa diwani kwa kipindi kilichopita ambaye kasema kuwa lengo ni kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Bukoba mjini.
Bi Christine Rwezahula ni mwanamke ambaye amejitosa katika kinyanganyiro cha kuwania kuipeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya ubunge jimbo la Bukoba mjini ambapo amesema kuwa anaamini chama kimewapa nafasi kubwa wananwake katika nafasi za utawala hivyo ameona anafaa kugombea ubunge katika jimbo hilo.
Ameongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa katika chama chao hivyo kama chama kimewaamini sasa hawana sababu za kusita kugombea nafasi za uongozi na kuwatumikia watanzania.
Mwingine ni aliyekuwa katibu wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Kagera Bukoba Ndg.Kilwanila Kiiza, Ndg. Valeriani Rugarabamu na wengine wengi.