Bosi wa G Unit, 50 Cent ameiponda albam mpya ya Jay Z iliyopewa jina la 4:44 akidai ni sawa na kusikiliza lugha rasmi ya wasomi wa chuo kikuu.
Rapa huyo ambaye aliwahi kuwa hasimu wa Jigga miaka kadhaa iliyopita ametumia mtandao wa Instagram kurusha makombora yake akidai albam hiyo inapaswa kusikilizwa kwenye viwanja vya mchezo wa golf.
“Nilihisi kama nilipaswa kuwa nimevalia miwani na tai, sweta kiunoni. Ni kama nasikiliza hotuba ya lugha rasmi ya wasomi (Ivy language). Ilikuwa kama muziki wa golf,” yanasomeka baadhi ya maandishi ya 50 kwa tafsiri isiyo rasmi.
Aliongeza kuwa hata mashabiki wa muziki ambao wako naye muda huo hawataki kusikiliza albam hiyo bali wanataka kuwa na wakati mzuri zaidi.
50 alienda mbali zaidi katika kumshambulia HOV akidai kuwa Jay Z hawezi kushindana na wasanii wapya kwa sababu ameshazeeka, huku akitaja mfano wa bifu la hivi karibuni kati ya nguli huyo na rapa Future.
“Huwezi kuwa rapa bora zaidi ukiwa na umri wa miaka 47, kwa sababu marapa wapya wako hapa. Wanakuja na vitu vipya. Ndio maana nilikuwa nacheka na Joe Badden na Migos kwa sababu wako hatua nyingine. Unatakiwa kuwaacha marapa vijana waingie. Unazinguana na Future na mambo mengine, muache jamaa,” ni tafsiri isiyo rasmi ya alichokiandika 50 kwenye Instagram.
Jigga na 50 wamewahi kuwana uhasimu unaokolea na kufifia tangu mwaka 1999 baada ya kiongozi huyo wa G-Unit kuanza kumchana Hov.
- Wema Sepetu awaonya wajawazito kupiga picha za utupu
Ingawa bifu lao limeendea, kumewahi kuwa na wakati ambapo amani ilitawala. Mwaka 2007, 50 Cent alimualika Jay Z na P. Diddy kwenye hafla ya kusherehekea kutajwa kuwa wasanii wa hip hop watatu wenye fedha nyingi zaidi (Hip-Hop Cash Kings).
Mwezi uliopita, Jay Z alimtaka 50 kuwa kati ya wachenguaji walimhamasisha kwenye safari yake ya muziki na heshima aliyonayo.