Aliyekuwa Miss Tanzania 2006, ambaye kwa sasa ni muigizaji wa Bongo movie, Wema Sepetu amewatolea uvivu wanawake wote wenye mimba wanaopiga picha za utupu kuonesha matumbo yao wakiwa wajawazito.

Wema Sepetu amewapaka wanawake hao na kusema kuwa waache kuweka picha za matumbo yao yenye mistari ya ujauzito.

”Muache kutuwekea mipicha ya mitumbo yenu yenye mstari ya ujauzito” ameandika Wema Sepetu kupitia ukarasa wake wa Instagram.

Hata hivyo mrembo huyo hakutaka kuwaacha salama wanawake wenye tabia hiyo, amewaonya kuacha kuiga tamaduni za kizungu na kutakiwa kudumisha na kuzienzi tamaduni zao za kiafrika zinazowata kujistili.

Aidha ya yote Wema Sepetu alianza kwa kujikubali kuwa yeye sio mwanamke wa kwanza kutojaaliwa mtoto, lakini sio sababu ya yeye kuacha kusema ukweli pale anapoona mambo hayaendi sawa.

Wema alichukua nafasi hiyo kumpongeza Esha Buheti kwa kuwa tofauti na wanawake wengine baada ya kuposti picha yake akiwa mjamzito huku amejistili.

 

Bavicha watoa neno kwa wateule wa JPM
Ali Kiba amsainisha Ommy Dimpoz RockStar4000