Takriban watu 600 wamejitokeza kufuata huduma ya uzazi pandikizi tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma Pandikizi (IVF), cha Hubert Kairuki cha jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa hii leo Februari 6, 2023 na Mtendaji Mkuu wa kituo hicho, Dkt. Clementina Kairuki amesema wanalenga kuhakikisha huduma bora za uzazi pandikizi zinawafikia Watanzania walio wengi kwa gharama kati ya Shilingi 13-15 milioni kutegemeana na vifaa na dawa.
Amesema, “Kati ya hawa 45 tayari 35 wameshapata ujauzito, kwa hiyo tunakwenda vizuri maana huduma hii matokeo yake yanaweza yasiwe kwa asilimia 100 lakini kwa kuwa sisi ndiyo tumeanza na tumepata matokeo hayo inaleta matumaini.”
Jumla ya Shilingi 4.5 bilioni, zimetumika kufanya uwekezaji wa ujenzi, miundombinu na vifaa tiba ya kituo hicho, kikiwa na uwezo wa kufanya upandikizaji kwa watu 1,000 kwa mwaka.