Jeshi la Polisi Mkoani Tanga, linaendelea na msako wa kuwatafuta na kuwakamata watu ambao walifanya tukio la wizi wa vyakula na mali nyingine katika ajali iliyotokea Februari 4, 2023 ikifusisha Lori na Basi dogo la abiria na kusababisha vifo vya watu 18 papo hapo.

Agizo la msako huo, limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba wakati wa shughuli za kuaga miili ya marehemu zilizofanyika katika Hospitali ya Magunga iliyopo Wilayani Korogwe na kuongeza kuwa jambo hilo si jema na linatakiwa kukemewa.

 Muonekano wa Basi dogo lililolkuwa liimebeba mwili wa Marehemu kwenda kuzika mkoani Kilimanjaro baada ya kupata ajali.

Alisema, “Kwa waokoaji kwenda kuwaokoa majeruhi, kwa kutoa miili pia kwenda kuwaibia, Jeshi la Polisi lipo watafuteni kwa njia zozote zile waliofanya vitendo vya kiharamu tunawatia nguvuni na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.”

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo ilifikia 20 baada ya majeruhi wengine wawili kufariki wakiwa wanapatiwa matibabu, mmoja katika Hospitali ya rufaa Bombo iliyopo Mkoani Tanga na mwingine Hospitali ya Taifa Muhimbili ya Mkoani Dar es Salaam.

Joto la uchaguzi lazidi kupanda, BVAS kutumika
CCM haikushinda uchaguzi 2020: Lissu