Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba ametoa taarifa ya majeruhi wengine wawili kufariki dunia leo Februari 5, 2023, wakati wakipatiwa matibabu.

Wawili hao wamefariki wakati mmoja wao akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bombo Mkoani Tanga, na mwingine Hospitali ya Taifa Muhimbili ya Mkoani Dar es Salaam.

Ajali hiyo, ilitokea jana Februari 4, 2023 wakati wanasafirisha mwili kwenda kuzikwa mkoani Kilimanjaro ambapo 18 walifariki papo hapo baada ya ajali iliyotokea wilayani Korogwe mkoani Tanga ikihusisha gari ya mizigo ‘Fuso’ na Coaster.

“Tutavunja itifaki kidogo kutokana na kuongezeka idadi ya waliofariki, itabidi tukiendelea na ibada tusubiri miili mingine miwili kutoka Tanga ambayo majeruhi wengine wamefariki.”amesema Mgumba.

Kutokana na kuongezeka kwa idadi hiyo ya vifo, jumla ya vifo kwa sasa inafikia 21 ukiongeza na marehemu aliyekuwa akisafirishwa.

Tisa wakiwemo Viongozi wa siasa mbaroni kwa kulima bangi
Jenerali Pervez Musharraf afariki dunia