Takribani watu 17 wamefariki na wengine 12 kujeruhiwa baada ya Basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana na Lori uso kwa uso usiku wa kuamkia Februari 4, 2023 Korogwe Mkoani Tanga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema ajali hiyo imetokea barabara ya Segera – Buiko iliyopo katika eneo na Kata ya Magira Gereza, Mombo Wilayani Korogwe ikihusisha Lori aina ya Mitsubishi Fuso na Basi dogo aina ya Coaster.

Muonekano wa Basi dogo la abiria aina ya Coaster lililopata ajali.

Amesema, “miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo na wengine wawili wamebaki Hospitali ya Korogwe kwa matibabu.”

Aidha, amesema Basi hilo dogo lilibeba mwili wa marehemu na abiria 26 na lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Moshi kwenye mazishi, huku chanjo cha ajali hiyo kikiwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa fuso aliyekuwa akilipita gari la mbele yake bila ya kuchukua tahadhari.

Rais Dkt. Samia ateua wengine saba
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 4, 2023