Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump wametoa heshima zao za mwisho kwa Rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye eneo maalumu lijulikanalo kama Capitol Rotunda ndani ya bunge jijini Washington DC.
Trump na mkewe walisimama kwa takribani dakika moja kabla ya Rais Trump kumpigia saluti marehemu Bush na kisha Trump aligeuka na kuondoka na mkewe.
Jengo la bunge lipo wazi kwa ajili ya waheshimiwa na raia wa kawaida kutoa heshima zao hadi Jumatano, huku wageni nao wakiruhusiwa kuzunguka mahala lilipowekwa jeneza.
Aidha, Rais huyo wa zamani wa Marekani alifariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 94 akiwa nyumbani kwake kwenye jimbo la Texas nchini Marekani baada ya afya yake kuzorota kwa miaka kadhaa.
-
Suala la ushoga kwa ‘Makasisi’ lampa wasiwasi Papa Francis
-
UN yaonya kuhusu ongezeko la joto duniani
-
Polisi wataka Netanyahu ashtakiwe
Hata hivyo, mtoto wa kiume wa Rais wa zamani wa 41 ambaye pia alikuwa Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush alionekana mwenye huzuni wakati alipoliangalia jeneza la baba yake mzazi lilipowekwa kwenye eneo maalumu kwenye Capitol Rotunda.