Mwanamziki na mtangazaji wa The Nick Cannon Show Nicholas Scott Cannon ameibuka kupitia instagram yake na kuandika kwamba ataendelea kuyaenzi ambayo Nipsey ameyaacha ikiwemo hili la kuiachia makala ya Dr. Sebi.

Masaa 24 baada ya kifo cha mwanaharakati na mwanamuziki wa Rap Nipsey Hussle mengi yamezungumzwa ambapo serikali ya Marekani imehusishwa na mauaji hayo..

Wengi wanaamini kwamba Nipsey ameuawa kutokana na harakati zake za kutaka kuiachia Makala ambayo inaeleza kwa kina tiba ya dawa ya virusi vya Ukimwi (AIDS) pamoja na saratani dawa ambayo iligunduliwa na Dr.Sebi.

Hata hivyo kuachiwa kwa Makala hiyo na kuiweka wazi dawa ya HIV AIDS kungepelekea serikali ya Marekani kukosa fedha ambazo tayari inaingiza kwa kutegeneza kinga pamoja na dawa za kupunguza makali, Nipsey alikuwa akiweka wazi juhdi za kutaka kuachia Makala hiyo na ndiyo inatajwa kuwa chanzo cha kifo chake.

Aidha Nick Cannon amesisitiza na kusema kuwa hawawezi kutuuwa wote ”Cant kill us all” ataimaliza na kuiachia Makala hiyo.

Polisi yamsaka 'Eric Holder' kwa udi na uvumba kuhusika kifo cha Nipsey
Serikali yatoa tahadhari kwa wananchi wanaofanya biashara ya kubadilisha fedha