Watu watatu ambao ni raia wa China Li Ninchui, Wang Xialing na Wang Zungusong wamekamatwa wakiwa na vifurushi 9 vya Sulphate na box moja ndani vikiwa na mawe ya madini na walipohojiwa kuhusu nyaraka za mawe hayo na vibali hawakuwa navyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe amesema kuwa tukio hilo lilitokea Juni,12, 2019 majira ya saa saba mchana katika barabara ya Sirari-Musoma eneo la Nkende walikamatwa na Askari wa usalama barabarani wakiwa Na gari KBW 515L Toyota Cruiser .
“Tumefanya taratibu za sampuli zikachukuliwa na kupelekwa kwenye maabara ya Madini Dodoma, majibu yalitoka na kubaini kuwa mawe hayo yana madini ya Dhahabu, Aluminium Oxide, Silicon Oxide, Calcium,Titanium, Magnesia na Madini mengine yenye viwango tofauti tofauti,”amesema Kamanda Mwaibambe
Amesema kuwa watuhumiwa hao wamefikishwa Mahakamani kwa makosa 2 ya kupatikana na Madini bila kibali, Uhujumu Uchumi na utoroshaji wa Fedha kesi Na. 27/2019 na wako rumande kesi yao itatajwa Julai,5,2019.
Wakati huohuo, Juma Thomas Makuri (37) mlinzi katika kampuni ya ulinzi iitwayo Alpha Security, aliyekuwa analinda kwenye Hotel JM ambapo ulitokea wizi wa TV na uchunguzi ulipofanyika iligundulika ndiye aliyeiba akishirikiana na mlinzi mwenzake.
Mwaibambe amesema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alikiri kutenda kosa nakwenda kuwaonyesha TV kati ya tatu alizochukua ambapo zingine zimeshauzwa na kwamba 2011 mtuhumiwa huyo alifungwa miaka 5 kwa kosa la wizi wa pikipiki na kutoka 2013 kwa msamaha.