Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Singida, Adili Elinipenda kumkamata Afisa manunuzi wa chuo cha ualimu Kinampanda, Francis Muyombo kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali kwa kughushi nyaraka.
Hayo yamejiri wakati Waziri akikagua ukarabati wa majengo ya chuo hicho kilichopo wilayani Iramba.
Ambapo alibainisha kughushi kwa nyaraka za vifaa vya ujenzi kunuliwa kwenye duka la nguo, pia alibaini udanganyifu mkubwa uliofanyika kwenye gharama za manunuzi ambapo kitasa kimoja kilioneshwa kimenunuliwa kwa elfu sabini huku bei halali ya kitasa hiko kuwa ni shilingi elfu ishirini na tano.
”Mmeenda kununua kitasa kwa Kisaka, afu Kisaka ni duka la nguo sio duka la hardwear na vitasa hivi vyote ni shilingi ishirini na tano elfu si elfu 70 kama mlivyonyesha hapa”. amehoji Waziri.
Hivyo, Waziri alimuamuru RPC kumuweka ndani Kisaka ambaye amehusika katika udanganyifu ho kwa kutoa risiti hizo feki zilizoonyesha manunuzi ya vifaa vya ujenzi kwenye duka la nguo.
‘RPC yupo nenda kamata mtu anaitwa Kisaka huko mjini, muweke ndani tutapa maelezo yote kwa Takukuru” aliamuru Waziri Majaliwa.
Katika ukaguzi alioufanya amebaini nyaraka zinazoonyesha kuwa kitasa kimoja kimenunuliwa kwa shilingi elfu sabini huku gharama halali ya kitasa kilichonunuliwa na kufungwa kwenye milango ni shilingi elfu ishirini na tano.
Mara baada ya kumuhoji afisa huyo anayehusika na manunuzi na kukuta hana maelezo ya kujitosheleza kuelezea sakata hilo, Waziri aliamuru akamatwe awekwe ndani kwa maelezo zaidi.
Aidha, Waziri amezunguma kuwa Kati ya mambo ambayo hayahitajiki ni udanganyifu amesema ni lazima watu wazingatie suala zima la pesa na thamani ya vitu vinavyonunuliwa na pesa hiyo, hivyo amewaamba watanzania kuacha udanganyifu huu ambao umekuwa unajitokeza mara kwa mara wakati wa kusimamia miradi ya serikali kwa ajili ya wananchi wao.