Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ametoa agizo kwa mkuu  wa  Jeshi la  Polisi  Nchini, IGP  Simon  Sirro  kutuma timu ya wataalamu kutoka Makao  Makuu  ya  jeshi ili kufika wilayani Ikungi ikiwa ni kuharakisha  Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Wilayani hapo sambamba na chumba cha mahabusu ambacho si sahihi kiafya kwa matumizi ya binadamu.

Ameyasema  hayo  baada  ya  kutembelea  kituo chakavu na ofisi za polisi wilayani hapo ikiwa ni ombi la mbunge wa  Singida  Mashariki, Miraji Mtaturu  aliloomba  katika  Bunge  lililoisha  hivi karibuni.

Akizungumza katika ziara hiyo Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu amesema anaishukuru serikali kusikia ombi lake huku akiweka wazi hali mbaya katika kituo hicho.

Naye mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogoro amesema uwepo wa kituo hicho kipya kikikamilika kitaimarisha Ulinzi na Usalama wilayani hapo.

Lamine Moro, Ally Ally, Banka kuikabili JKT Tanzania
Ndemla atakiwa Singida UTD kwa mkopo.