Kocha Mkuu wa Singida United Nsanzurwimo Ramadhani ameonyesha nia kumtaka kwa mkopo kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla, ambaye amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Tanzania bara.

Singida United imekuwa na wakati mgumu msimu huu kwani mpaka sasa  inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imejikusanyia alama nne tu.

Nsanzurwimo amesema wamedhamiria kuhakikisha wanaibakisha timu hiyo ligi kuu, hivyo watatumia usajili wa dirisha dogo kusajili nyota wenye uwezo.

Hata hivyo changamoto za kiuchumi zilizoikumba timu hiyo huenda zikawafanya washindwe kuipata huduma ya Ndemla, kutokana na masharti yaliyowekwa na Simba kwa timu zinazowataka wachezaji wake kwa mkopo.

Hivi karibuni Mtendaji wa Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa alisema timu yoyote inayomtaka mchezaji wa Simba kwa mkopo lazima ithibitishe kuwa na uwezo wa kumlipa mshahara wake anaolipwa Simba kwa muda wote atakaoichezea timu hiyo.

Alisisitiza Simba haitakuwa tayari kuingia gharama ya kulipa mishahara ya wachezaji ambao wanazichezea timu nyingine kwa mkopo.

Klabu ya KMC nayo inamuwania kwa mkopo winga Rashid Juma.

Timu ya IGP Sirro yatakiwa kutinga Ikungi, ujenzi kituo cha Polisi
Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki waanza