Mabingwa mara 27, wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans wapo tayari kuwavaa Maafande wa JKT Tanzania kesho katika mchezo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo kwenye mkutani na waandishi wa habari uliofanyika leo mchana makao makuu ya klabu, jijini Dar es salaam, Afisa habari na mawasiliano wa Young Africans, Hassan Bumbuli amesema kwa mujibu wa kocha wao, Charles Mkwasa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo huo.

Bumbuli amesema licha ya mabadiliko ya ratiba, kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo, huku akikiri uwezekano wa kuwakosa baadhi ya wachezaji wao muhimu.

“Viongozi wa mpira ni wao lakini sisi ndio wadau wakubwa, wanapobadili ratiba ni lazima wafanye mawasiliano na klabu maana sisi ndio tunaocheza sio wao,” amesema

“Haiwezekani wanabadili ratiba bila kuhushisha vilabu kwanza ambavyo ndio wadau wakubwa na ndio wenye mechi”

Akizungumzia viingilio vya mchezo huo, mhamasishaji wa Young Africans, Antonio Nugaz amesema Shilingi 10,000 kwa jukwaa kuu, mzunguko ni Shilingi 5,000.”

Nugaz ameongeza kwa kuwataka wadau na mashabiki wa Young Africans kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuisapoti timu hiyo kupata matokeo ya ushindi.

Michezo mingine ya ligi kuu ya soka Tanzania bara itakayochezwa kesho ijumaa itashuhudia:

Tanzania Prisons v Mwadui FC (Sokoine Stadium, Mbeya)

Namungo FC v Coastal Union (Majaliwa Stadium, Luangwa – Lindi)

Ndanda FC v Polisi Tanzania (Nangwanda Sijaona, Mtwara)

Kagera Sugar v Lipuli FC      (Kaitaba Stadium, Bukoba – Kagera)

Alliance FC v KMC FC (Nyamagana, Mwanza)

 

Ligi kuu itaendelea tena keshokutwa jumamosi kw amichezo kadhaa kuchezwa ambapo

Biashara United v Mtibwa Sugar (Karume Stadium, Musoma-Mara)

Mbao FC v Azam FC (CCM Kirumba, Mwanza)

Mbeya City v Singida United (Sokoine, Mbeya)

Ruvu Shooting v Simba SC (Uhuru Stadium, Dsm)

Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki waanza
Baba Levo aachiwa huru, Zitto atoa neno