Watu 14 wamepoteza maisha na wengine wanne wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wanasafiria kulipuliwa kwa bomu, Kusini-Magharibi mwa Burkina Faso.
Basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi waliokuwa wanarejea mashuleni baada ya kumaliza mapumziko ya sikukuu za kuukaribisha mwaka mpya 2020.
Taarifa zilizotolewa na vyombo vya usalama nchini humo zimeeleza kuwa basi hilo lilikanyaga bomu katika eneo la Toeni.
Ingawa bado watuhumiwa wa tukio hilo hawajafahamika, nchini humo kumekuwa na ongezeko la tishio la makundi ya kigaidi.
Katika siku ya Christmas, raia 35 waliuawa katika matukio ambayo yalidaiwa kutekelezwa na makundi ya kigaidi dhidi ya kambi za jeshi.
Nchi za Afrika Magharibi zimeendelea kupambana na vitisho vya kigaidi lakini mauaji na vitendo vya kigaidi vinaendelea.