Kikongwe mwenye umri wa miaka 80, Obed Ndosi, maarufu kama Ulong’a, mkazi wa kijiji cha Masama Mbweera, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya Hai mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na shtaka la kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Ulong’a anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha kifungu 130 na 131 cha sheria iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Mwendesha mashtaka wa serikali Lobulu Mbise, aliposoma hati ya mashtaka amesema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13, katika kijiji cha Masama Mbweera Desemba 8 mwaka jana kwa nyakati tofauti.

Kesi hiyo namba 333 ya mwaka 2019, inasikilizwa na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo, Devotha Msofe.

Baada ya mshtakiwa kusomewa mashtaka hayo, alikana kutenda kosa hilo na hakimu aliahirisha shauri hilo hadi Januari 29, mwaka huu kesi hiyo itakapo tajwa tena.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Serikali, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Hakimu alisema dhamana ya mshtakiwa huyo ipo wazi na kwamba alitakiwa kuweka bondi ya sh. milioni tano. Hata hivyo mshtakiwa alitimiza matakwa ya dahamana na kuachiwa.

Wanafunzi wauawa kwa bomu wakiwa ndani ya basi
Kichaa amuua mtoto kwa kumgongesha kwenye gogo