Polisi nchini Uganda wamemkamata Kiongozi wa vuguvugu la ‘People Power’, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine na baadhi ya viongozi wake wengine.

Bobi Wine ambaye ni Mbunge wa Kyadondo Mashariki amekamatwa baada ya Polisi kufyatua mabomu ya machozi na risasi za moto kutawanya Wapinzani katika mkutano wao.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika katika Shule ya Sekondari Our Lady of Good Counsel huko Kyadondo Mashariki ambapo Wine alitarajia kueleza mipango yake kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2021.

Polisi waliwazuia watu kuingia Ukumbini na kuwakamata Wine na timu yake ambapo wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kisangati.

Australia: Hali yazidi kuwa Ngumu, Moto wateketeza ekari mil.15, wanyama na vifo vya watu
Mtoto wa miaka 1o ajitahiri kwa kisu