Idadi ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda imeongezeka na kufikia 23 kutoka 18 baada ya watu wengine watano kukutwa na maambukizi siku ya Ijumaa.
Dkt. Jane Ruth Aceng amesema kuwa kati ya sampuli 227 zilizofanyiwa vipimo siku ya Ijumaa watu 222 hawakupatikana na virusi vya corona huku watu watano wakipatikana na ugonjwa huo, katika chapisho lake la mtandao wa twitter.
”Waganda tafadhalini fuateni maelezo na mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivi Tunaweza kuzuia maambukizi ya virusi hivi pamoja”, amesema afisa hiuyo.
Ikumbukwe kuwa Rais Museveni alisema kwamba kutokana na visa hivyo vipya huenda kukawa na umhimu wa kuchukua hatua kali zaidi ili kuzuia maambukizi kulingana na ujumbe wa twitter uliotumwa na katibu wake wa maswala ya habari, Don wanyama .
Maafisa wa afya wanasema kwamba watu wote 14 waliothibitishwa hapo awali kuwa na virusi hivyo wanaedlea vyema katika hopsitali ya Entebe Grade B , Hospitali ya Mulago na hospitali kuu ya Adjumani.