Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa mikoa 7 ya kanda ya pwani na kanda ya kati ya Tanzania kutokana na uwezekano wa kunyesha mvua za wastani na kubwa kwa baadhi ya maeneo
Taarifa ya TMA imesema “mikoa ifuatayo itarajie mvua kubwa na wastani kwa takribani siku tano kuanzia April 12 mpaka tarehe 17 April, wakazi wa mikoa hii wanatakiwa kuchukua tahadhari kutokana na hali hii ya mvua”.
Mikoa hiyo ni Dar es salaam, Tanga, Lindi, Morogoro, Pwani visiwa vya Mafia,Unguja na Pemba, hata hivyo Tangu siku ya jana mkoani Dar es salaam mvua imekuwa ikinyesha kwa takribani masaa kadhaa hali iliyosababisha baadhi ya barabara kufungwa na usafiri kuchelewa.
Aidha athari za mvua hizo ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadi ya shughuli za kiuchumi na jamii , kuzama kwa baadhi ya vyombo majini pamoja na kuathiri kwa shughuli za uvuvi na usafirishaji