Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametuma salamu za sikuku ya pasaka na kuwataka wananchi kuepuka mikusanyiko.

Waziri Ummy ametuma ujumbe huo leo kupitia ukurasa wake wa twitter huku akisisitiza Corona inazuilika ni muhimu kuzingatia maelekezo ya wataalamu.

“Heri ya pasaka. Baki salama. Corona inazuilika. Epuka mikusanyiko. Tuwalinde watoto na wazee. # jikingeWakingeWengine,” amesema Waziri.

Waziri ummy amesisitiza kuwa ”Tusherehekee kwa amani na utulivu huku tukiepuka mikusanyiko isiyo ya lazima”.

Aidha, amesema kusherehekea sikuku ya Pasaka  kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu  wa afya ili kujikinga na ugonjwa huo.

Dk.Shoo : "Tumtegemee Mungu na kufuata maelekezo kuhusu Corona"
WHO kutafiti sababu waliopona Corona kuumwa tena