Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Upendo Peneza ameiomba Serikali ichukue hatua ya kupiga marufuku watu wa jiji la Dar es Salaam kutoka kwenda maeneo mengine ya nchi amabayo bado hayajathirika vikali na COVID 19.

Amesema kuwa kama hatua stahiki hazitachukuliwa juu ya ugonjwa huu kwa umakini mkubwa basi ugonjwa huo utasambaa kwa kasi sana.

Hivyo ameomba wakazi wa Dar Es Salaam wazuiliwe kutoka kwenda maeneo mengine huku huduma za msingi kama vile chakula zikitolewa katika utaratibu maalumu utakaozingatia tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema hayo leo Aprili 16, 2020Ā  bungeni jijini Dodoma akidai kuwa ni vyema tahadhari zikachukuliwa mapema kabla ya ugonjwa huo kusambaa kwa watu wengi zaidi kwani nchi haina uwezo mkubwa wa kukabiliana na ugonjwa huo hivyo ni vizuri kuuwahi kabla mambo hayajawa makubwa zaidi.

Aidha, takwimu zinaonyesha kuwa mpaka sasa jiji la Dar es Salaam kinara kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 kulinganisha na mikoa mingine Tanzania, ambapo Dar es salaam kuna visa 62, Arusha visa vitatu, Kilimanjaro kisa kimoja, Kagera kisa kimoja, Mwanza visa vitatu na Zanzibar visa 13.

Idadi hiyo inafanya Tanzania kuwa tayari imeripoti visa 88, ambapo wagonjwa waliopona mpaka sasa wafikia 11 na kupatikana kwa vifo vinne.

Ā 

Visa vya Corona Tanzania vyafika 94, Wengine 6 wakutwa ''Positive''
Peneza aitaka Serikali iwasaidie wafanyabiashara walioathirika na COVID 19