Chuo kikuu cha Johns Hopkins kikiwa kinaendelea kutoa takwimu za kidunia kuhusiana na mwenendo wa ugonjwa wa COVID 19 ambapo hadi kufikia leo takwimu zinaeleza dunia imekumbwa na jumla ya vifo zaidi ya laki moja (137,078) huku jumla ya visa vilivyothibitishwa kufikia milioni mbili na zaidi.

Ambapo nchi ya Marekani inashika kinara kwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya virusi hivi kwani watu takribani laki sita (638,455) wamethibitika kuathirika na virusi vya corona huku kukiwa na vifo zaidi ya elfu thelathini (30,921).

Ikifuatiwa na nchi ya Uhispania inayoshika nafasi ya pili kwa maambukizi ya watu wengi ambapo watu takribani 180,659 wameripotiwa kuathirika, huku vifo vikitajwa kuwa 18,812.

Nafasi ya tatu ikishikiliwa na nchi ya Italia ambayo tayari imeripoti idadi ya watu 165,155 wakiwa ni waathirika na jumla ya idadi ya vifo 21, 654.

Ujerumani nayo ina idadi kubwa ya maambukizi ambapo visa vilivyotangazwa mpaka sasa ni 134,753, na wakiwa na vifo 3,804 ambayo ni idadi ndogo kulinganisha na idadi ya waathirika.

Ufaransa nayo hali si shwari kwani inaripotiwa kuwa na visa 133,740 pamoja na vifo 17,167.

Kwa upande wa Afrika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kinara kwa vifo kwani hadi sasa watu takribani 24 wamepoteza maisha huku waathirika wakiwa wamefikia 254.

Aida, Tanzania hadi kufikia mchana wa leo Aprili 16, 2020 tayari visa 94 vimeripotiwa na kuwepo na vifo vinne tu huku watu 11 wakiripotiwa kuwa wamepona.

Zidane amvutia kasi Aubameyang
Muhimbili yaokoa maisha watoto wanaozaliwa utumbo nje