Mabingwa wa kihistoria barani Ulaya klabu ya Real Madrid, wameripotiwa kuwa katika mpango wa kumsajili mshambuliaji wa washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang.

Aubameyang amekua katika vichwa vya habari za michezo katika kipindi hiki, kufuatia klabu kadhaa kutajwa kutamani kumsajili itakapofika wakati wa majira kiangazi, jambo ambalo limeendelea kuonyesha huenda akapanda thamani.

Real Madrid wanatajwa kuwa katika mipango ya kusajili mshambuliaji huyo kutoka Gabon, ili kutimiza haja yao ya kuziba pengo lililoachwa wazi na Cristiano Ronaldo, ambaye alitimkia kwa mabingwa wa Italia Juventus mwaka 2018.

Meneja wa wababe hao wa mji wa Madrid Zinedine Zidane, anaamini Aubameyang anaweza kuziba pengo lililoachwa na Ronaldo, kutokana na umahiri wake anaoendelea kuuonyesha akiwa na Arsenal, iliyomsajili Januari 2018 akitokea Borussia Dortmund.

Kama itakumbukwa vyema mwishoni mwa juma lililopita, Rais wa Chama cha Soka cha Gabon (FEGAFOOT) Pierre Alain Mounguengui alimshauri Aubameyang kuhamia kwenye klabu yenye matamanio makubwa zaidi ya kupata mafanikio tofauti na Arsenal.

Alipohojiwa na ESPN Pierre Alain Mounguengui alisema: “Sitaki kusema Arsenal hawana matamanio , lakini Arsenal hawana matamanio makubwa kama vilabu vingine vikubwa barani Ulaya.”

“Kama Pierre ataweza kupata uhamisho kwenye klabu yenye matamanio zaidi , basi bila shaka atakuwa na nafasi yake katika hiyo klabu. Tunamuona yeye kuwa mmoja wa washambuliaji bora Duniani.”

“Lakini ushauri ninaotaka kumpa ni yeye kuendelea kufanya kazi kwa juhudi kubwa na kuvutia vilabu vikubwa vyenye matamanio makubwa zaidi”

Gwiji wa Arsenla Ian Wright naye alisema, “Kama ukimfikiria Aubameyang kwenye timu nzuri zaidi basi atakuwa anatwaa mataji na kuwania nafasi za kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na nafikiri anastahili hilo.”

Kama ukitoa magoli yake katika ile timu basi watakuwa kwenye matatizo makubwa sana . Arsenal wanahitaji wachezaji kadhaa kuwa katika ubora wao ili kumsaidia Pierre.”

Sukari kutoka nje yatua Tanzania kuokoa jahazi
Mwenendo wa Corona Duniani, visa vyafika 2,064,833, vifo 137,078