Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford amesema alivumilia kipindi kigumu chini ya aliyekua meneja wa klabu hiyo ya Old Trafford Jose Mourihno, na kufanikiwa kuwa mchezaji bora.

Mourihno alikuwa meneja wa Manchester United kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 na kufanikiwa kutwaa taji la Europa na kombe la Ligi (Carabao Cup) katika Msimu wake wa kwanza akiwa Old Trafford.

Akiwa na Manchester United Mourihno mara nyingi alikuwa anakosolewa mifumo aliyokuwa anaitumia na kutokuwa na maelewano na wachezaji muhimu kama Paul Pogba.

Rashford alipachika mabao 28 na kutoa pasi za mwisho 20 chini ya meneja huyo kutoka nchini Ureno, ambaye hivi sasa ni meneja wa Tottenham Hotspurs.

Mshambuliaji huyo kutoka England alionesha kiwango kizuri chini ya Mourihno na anashukuru kwa uzoefu alioupata chini ya mreno huyo, ambaye kwa sasa amepoteza mvuto.

Tangu Mourihno alipofungashiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Ole Gunner Solskjaer bado Rashford amendelea kuwasha moto amecheka na nyavu mara 19 katika mechi 31, alishuka dimbani msimu huu akiwa na Manchester United. Kama asingepata majeraha ni dhahir angekuwa kwenye kilele cha wafungaji bora kama Vardy, Auba na Aguero.

GSM kuzalisha zaidi ya jezi Young Africans
Ujerumani: Biashara zafunguliwa baada ya mwezi mmoja wa karantini