Ujerumani imeanza hatua ya kuruhusu kufunguliwa kwa baadhi ya biashara ikiwa ni awamu mpya huku shule zikitarajiwa kufunguliwa mwezi mei katika hatua zake za kupambana na janga la kuenea kwa virusi vya Corona.

Hatua hiyo inatekelezwa baada ya shughuli nyingi za kibiashara kufungwa kwa mwezi mmoja huku awamu hii mpya maduka yanayoruhusiwa kufunguwa ni yale madogo na yale ya wastani, kwa nyakati tofauti na majimbo yote 16.

Ambapo kwa baadhi ya majimbo, maeneo mengine yatakayofunguliwa ni pamoja na sehemu ambazo wanyama wamehifadhiwa (Zoo). Shule zitafunguliwa kuruhusu watoto wa madarasa ya juu wanaotakiwa kufanya mitihani kujiandaa.

Hatua hiyo itafanyika katika majimbo ya Saxony, Berlin na Brandenburg. Shule nyingine zote zitafunguliwa mwanzoni mwa mwezi Mei.

Rashford ampa tano Jose Mourinho
KKKT yasitisha ibada dayosisi ya Karagwe