Papa Francis ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kubaki na mshikamano katika kukabiliana na athari za janga la virusi vya Corona.

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ametowa wito huo siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaojadili mpango mkubwa wa kiuchumi.

Aidha Papa Francis ameuomba Umoja huo kusali ili ufanikiwe kuuendeleza mshikamano wao wa miaka mingi.

Ufaransa yatoa msaada Tanzania kupambana na Corona

Janga la virusi vya Corona limesababisha mivutano mingine katika umoja huo wenye wanachama 27, na kwa mara nyingine kuonekana migawanyiko kati ya nchi tajiri za Ulaya Kaskazini na zile masikini kabisa za upande wa kusini.

Hata hivyo mara ya pili katika kipindi cha siku 10 kwa kiongozi huyo wa dini ambaye ni muungaji mkono mkubwa wa Umoja wa Ulaya kuzungumzia wasiwasi wake kuhusu Jumuiya hiyo.

Corona yawapandisha mume na mke kizimbani

Wakenya kupewa fedha za ruzuku ya athari za corona

Rais Magufuli ateua Makatibu Wakuu, Mganga Mkuu wa Serikali
Waziri Mkuu: Marufuku kupandisha bei ya vyakula mwezi Mtukufu wa Ramadhani