Nchi ya Ufaransa imesema kuwa imeazimia kuisaidia Afrika na Tanzania katika mapambana na maambukizi ya Covid-19 huku ikisisitiza kuwa imeweka nguvu zaidi kwenye nchi ambazo ziko hatarini zaidi.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kitengo Cha Mawasiliano cha Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania imeeleza kwa kina kuhusu nchi hiyo ilivyodhamiria kulisaidia Afrika na Tanzania dhidi ya ugonjwa huo.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frédéric Claivier kupitia taarifa hiyo amesema nchi ya Ufaransa imeamua kutumia njia mbalimbali zinazowezekana ili kulisaidia bara la Afrika na haswa nchi zilizo hatarini zaidi ili kupigana vita dhidi ya virusi vya COVID-19 katika bara la Afrika.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza Aprili 8, 2020 kutoa msaada wa pesa kiasi cha Euro (€) bilioni 1.2 ili kupambana na maambukizi ya Covid-19 barani Afrika.

Imeelezwa kuwa mpango wa “COVID-19 – “:Afya kwa Pamoja”, unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa
(AFD) utakusudia kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika na kuwajengea uwezo wanasayansi wa kiafrika katika kufanya gunduzi na tafiti mbalimbali za kisayansi.

Wakati huo huo amesema bado wanaendeleza mradi wa kilimo-ekolojia, unaotekelezwa na taasisi ya SwissAid pamoja
na asasi zisizo za kiserikali (NGOs) za Kitanzania ambazo ni SAT na TOAM zinalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo wapatao 6000, lengo likiwa kuzuia magonjwa ya mlipuko kwa watu waishio vijijini.

Pia kama sehemu ya Mpango wa “COVID-19 – Afya kwa Pamoja”, AFD imeahidi kuunga mkono serikali ya Tanzania kupitia mikopo yenye masharti nafuu ili kuiwezesha serikali kushughulikia changamoto za kiafya za muda mafupi na kwa wakati.

Balozi huyo wa Ufaransa nchini Tanzania pia amehamasisha kampuni za Ufaransa zilizopo nchini Tanzania kuunga mkono na kusaidia juhudi za serikali za kupambana na virusi vya corona kwa kutoa vifaa vinavyohitajika ili kupambana na ueneaji wa janga hilo.

Corona Marekani: vifo vyaongezeka, maambukizi yapungua
Jimbo la Marekani kuishtaki China kuhusu virusi vya corona