Mawaziri wanaohusika na masilahi ya wafanyakazi na ajira wa kundi la mataifa yaliyostawi kiuchumi duniani G20, wameahidi kulisaidia soko la ajira lisiporomoke wakati wa janga la virusi vya corona likiathiri kazi kote ulimwenguni.

Mawaziri wa kundi hilo ambalo kwa sasa linaongozwa na Saudi Arabia wamesema kwamba mataifa yao yataendelea kutafuta njia za kusaidia biashara na waajiri, hasa biashara ndogo ndogo, na za kati, ili kuokoa ajira na kusaidia wafanyakazi walioathirika katika kipindi hiki kigumu. 

 Jumanne Shirika la Kazi Duniani ILO lilionya kuwa athari za kiuchumi za mripuko wa virusi vya corona zinawaumiza vibaya wafanyakazi na waajiri katika sekta zote. 

 Lakini shirika hilo limesema kwamba wakati wowote vikwazo vikiondolewa, basi wafanyakazi wanapaswa kurudi kazini wakiwa na ulinzi sahihi, ili kuzuia kutokea tena kwa janga hilo.

Kenya kufanyiwa jaribio chanjo ya Corona
Wakenya waliopo China kurudishwa mei 1