Ikiwa imepita wiki moja baada ya Shirika la Afya duniani kuyaonya mataifa ya Ulaya kwamba bara la Afrika sio uwanja wa majaribio ya chanjo, tayari Nchi ya Kenya imependekezwa kufanyiwa.

Watafiti kutoka nchini Uingereza wanafikiria kufanyia majaribio chanjo ya virusi vya corona nchini Kenya ambapo kulingana na wao mlipuko wa ugonjwa huo unaongezeka.

Hatahivyo wanasayansi hao kutoka Chuo kikuu cha Oxford wanadaiwa kufikiria wazo hilo iwapo hawatopata matokeo ya haraka nchini Uingereza.

Mawaziri G20 kusaidia soko la ajira

Mkuu wa shirika la Afya duniani, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alilaani kauli alizoziita za “kibaguzi” kutoka kwa madaktari wawili wa Ufaransa ambao walitaka chanjo ya virusi vya corona kufanyiwa majaribio barani Afrika.

Hatahivyo imeelezwa kuwa kundi hilo la Oxford lina rekodi nzuri ya kipindi cha miaka 30 iliyopita ambapo limefanikiwa kutengeneza chanjo zilizofanikiwa dhidi ya aina nyengine ya virusi vya corona kama vile MERS, ambayo imefanikiwa katika majaribio yaliofanyiwa katika miili ya binadamu.

Mapema siku ya Alhamisi, majaribio ya kwanza katika mwili wa mwanadamu barani Ulaya yalianza Oxford.

Watu wawili waliojitolea, wote wakiwa wanasayansi walichomwa sindano ya chanjo na ndio watu wa kwanza kati ya zaidi ya watu 800 walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 55 ambao walichaguliwa kufanyiwa utafiti huo.

Profesa Tibaijuka: tiba asili si uchawi ni sayansi
Mawaziri G20 kusaidia soko la ajira